"Iran na Marekani zitakutana Oman siku ya Jumamosi kwa mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja ya ngazi ya juu," Araghchi amesema hayo katika ujumbe alioutuma kwenye mtandao wa kijamii X mapema leo Jumanne.
Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu ya Iran amesema mazungumzo hayo tarajiwa, "Ni fursa kubwa kama ambavyo pia ni mtihani. Mpira uko kwenye uwanja ya Marekani."
Kauli ya Araghchi imekuja baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kutangaza kuwa Marekani na Iran zitafanya "mazungumzo ya moja kwa moja" siku ya Jumamosi, baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu mjini Washington.
Hata hivyo, mkutano wa waandishi wa habari kati ya Trump na Netanyahu uliopangwa kufanyika jana Jumatatu katika Ofisi ya Oval ulifutwa, kwa mujibu wa Ikulu ya White House.
Rais wa Marekani alisema mazungumzo kati ya Washington na Tehran yatakuwa katika "ngazi ya juu sana." Hii ni katika hali ambayo, Trump anaitaka Tehran kuingia kwenye mazungumzo ya moja kwa moja kuhusu mpango wake wa nyuklia, huku akitishia kuivamia Iran kijeshi iwapo diplomasia itafeli.
Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anasisitiza kuwa, viongozi wa Marekani wana wajibu wa kuthibitisha kivitendo kuwa kweli wanataka mazungumzo na Tehran.
342/
Your Comment